Wanunuzi wadogo wa madini ya vito
Mkoani Arusha wameitaka Serikali kuwatambua na kuacha kuwanyanyasa kwa
kuwakamata mara kwa mara kwa madai ya kukosa leseni .
Wamedai kuwa wamekuwa wakifayiwa
vitendo hivyo kwa ni a ya kuwatisha kwa
lengo la kutoa nafasi kwa wanunuzi
wakubwa kitendo w alichokiita ni kuwakosesha fur sa wazawa .
Wametoa k auli hiyo katika kikao
cha kujadili matatizo yaliyosababisha baadhi yao kukamatwa kwa madai ya kukosa
leseni na kufanya biashara katika maeneo
yasiyo rasmi wakati wanaelewa kuwa hakuna sheria inayo wakataza na kwamba hiyo
ni mbinu ya kuwazima na kuwapa nafasi wanunuzi wakubwa .
Baadhi ya viongozi wa muungano wa
wanunuzi wadogo wa madini wamesema ,
kutokana na hali hiyo ,
wamekubalina na serikali kuwa kutakuwa na utaratibu maalum wa kufanya
biashara hiyo ambao utaanza kufuatw a hivi karibuni ili kuepusha mig ongano
iliyopo kati yao .
0 comments:
Post a Comment