FRORENCE
DYAULI amefariki dunia majira ya saa kumi alfajiri akiwa amelazwa katika
hospitali ya RABININSIA MEMORIAL jijini DSM ambako alikuwa akipata matibabu.
Dyauli
alizaliwa tarehe 27 mwezi wa saba mwaka
1961 na amefariki dunia tarehe 18/06/2015.
Marehemu
DYAULI alisoma shule ya msingi CHANG’OMBE mwaka 1968 hadi
1975.
Alipata
elimu ya sekondari mwa 1976 hadi 1979 katika shule ya wasichana KISUTU jijijini
DSM.
Baadae
alijiunga na Chuo cha Uhazili TABORA na kupata cheti katika fani ya katibu
muhtasi mwaka 1980 hadi 1981.
Marehemu
DYAULI alipata stashahada ya uandishi wa habari mwaka 1988 katika
chuo cha Uandishi wa habari TSJ jijini DSM.
Taratibu
za mipango ya mazishi tutaendelea kuwajulisha katika taarifa zetu zijazo.
0 comments:
Post a Comment