Image
Image

Uandikishaji wananchi katika daftari la wapiga kura laanza kisiwani Unguja.


Zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC limeanza Kisiwani UNGUJA huku wananchi wakijitokeza kwa wingi.
Changamoto hizo ni pamoja na upungufu wa mashine za kuandikisha katika baadhi ya vituo vya uandikishaji sambamba na upungufu wa vyumba vya uandikishaji kulingana na wingi wa watu wanahitaji kuandikishwa
Wakizungumzia kuhusu zoezi hilo , baadhi ya wakazi wa NUNGWI wamesema kuwa zoezi hilo limeanza vizuri lakini kuna umuhimu kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC kuangalia uwezekano wa kuboresha zaidi utoaji wa huduma hiyo kulingana na mahitaji ya watu wanaokwenda kujiandikisha.
Akitoa tathmini juu ya zoezi hilo Mwakilishi Mkuu Mkaazi kutoka UNDP PHILIPPE POINSOT yeye ameridhishwa kabisa na zoezi hilo na kuamini kuwa limezingatia taratibu za uandikishwaji wa watu .
Uandikishaji huo wa wananchi ndani ya daftari la kudumu la wapiga kura utajumuisha kwa wananchi wanaotakiwa kusajiliwa upya kutokana na kuhama eneo moja kwenda eneo jingine , wananchi watakaokuwa wamepoteza kadi zao hali kadhalika na wapiga kura wapya pia wataandikishwa
.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment