Recho amesema anaamini kuwa ni rahisi kwa
msichana mrembo na staa kama yeye kuendelea kuwa peke yake na kwamba huo ni
uamuzi wa mtu.
Amesema kwa sasa bado hana mwanaume
aliyemchagua kwaajili ya kutafuta familia na kuilea wakiwa pamoja kama mume na
mke.
“Bado nipo mwenyewe nafanya kazi, kwanza
wanaume wapo na endapo atapatikana kila mtu atafahamu lakini kwasasa bado nipo
mwenyewe natafuta maisha,” alisema.
Anasema sio kwamba hakuna wanaume
wanaompenda, wapo lakini bado hajaona mwanaume ambaye anaamini atakuwa mzazi bora
katika familia yake hapo baadaye.
0 comments:
Post a Comment