Serikali imesema itaendelea na
juhudi za kutatua tatizo la makazi kwa askari nje ya utaratibu wa kawaida wa
bajeti kwa ushirikiano na wadau mbalimbali chini ya mpango shirikishi wa PPP.
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi,PEREIRA AME SILIMA ametoa
kauli hiyo alipokuwa a kijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,CONCHESTA RWAMLAZA
aliyeuliza serikali ina mpango gani wa kuwapatia askari wa polisi na magereza
katika eneo la Nshambya na Miembeni
Manispaa ya Tabora nyumba bora kutokana na nyumba wanazoishi sasa kuchakaa.
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi,amesema jeshi la
polisi limepanga kulifanyia ukarabati jengo la ghorofa nne linalokaliwa na
familia 72 ililopo katika Manispaa ya Bukoba katika mwaka huu wa fedha endapo
serikali italipatia fedha hizo.
Wakati huo huo, Bunge limeelezwa
kuwa k atika kukabiliana na tatizo la kupanda na kushuka kwa bei ya mazao ya
biashara katika soko la dunia ikiwemo zao la tumbaku, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa mazao
inaandaa utaratibu wa kuanzisha mfuko maalum wa kufidia bei za mazao.
Naibu Waziri wa Kilimo,Chakula
na Ushirika,GODFREY ZAMBI amesemahayo alipokuwa a kijibu swali la
mbunge wa Mpanda Vijijini , MOSHI KAKOSO
aliyetaka kujua serikali inampango gani wa kuwafidia hasara waliyoipata
wakulima tumbaku walioathirika tatizo la kushuka bei kwenye soko la Dunia.
Naibu Waziri wa Kilimo , Chakula na
Ushirika amesema Waraka wa Baraza
la mawaziri kuhusu mapendekezo ya kutunga sheria ya kuanzisha mfuko wa kufidia
bei za mazao umewasilishwa katika ngazi
za u amuzi.
0 comments:
Post a Comment