Kufikia hatua hiyo Kenya iliitoa Cameroon katika nusu
fainali huku Algeria ikiitoa Senegal katika michezo inayoendelea katika viwanja
vya ndani vya Kasarani mjini Nairobi Kenya.
Kabla ya mechi ya fainali, Cameroon itavaana na
Senegal kumtafuta mshindi wa tatu.
Awali katika michezo ya makundi, Kenya iliibwaga
Algeria kwa seti 3-0.
Hata hivyo kocha wa timu ya Kenya David Lung'aho
amebainisha kuwa mchezo huo hautakuwa mwepesi kwani Algeria ni timu ngumu licha
ya kuifunga katika mchezo wa makundi.
Mpaka sasa Kenya imenyakua kombe la Afrika la Voliboli
kwa Wanawake mara nane, kwa mara ya kwanza ikilitwaa kombe hilo mwaka 1991 huko
Misri.
Timu nyingine zilizowahi kushinda kombe hilo ni Misri
na Tunisia mara tatu kila moja na Algeria ikiambulia mara moja mwaka 2009.
0 comments:
Post a Comment