Image
Image

Wanasiasa wakemea vikali mauaji yaliyofanywa katika kanisa la wamarekani wenye asili ya Afrika.


Shambulio lililosababisha mauaji ya watu wengi katika kanisa la Wamarekani wenye asili ya Afrika  limezua mjadala mkubwa ambapo wanasiasa wamekemea vikali mauaji yanayoendelea nchini humo hasa kwa  watu weusi.
Mgombea urais kwa tiketi wa Chama cha Democrat Bi HILLARY CLINTON amesema kwamba nchi hiyo inahitaji kurejelea sera zake na kutambua ukweli juu ya suala la ubaguzi wa rangi,umili ki wa  silaha na uhalifu.
Kijana wa Kizungu Dylann Roof mwenye umri miaka 21 anayeshukiwa ku fanya shambulio hilo amekamatwa  huku Rais BARACK OBAMA amesema kuwa mauaji ya watu ndani ya kanisa la Wamarekani weusi  Mjini   Charleston,Carolina ya Kusini kunaleta mfululizo wa mauaji yenye maswali mengi.
Baadhi ya raia wa kigeni na wale wenye asili ya Kiafrika waliopo nchini Marekani wanakumbwa na mashaka ya juu ya usalama wao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment