Waziri Mkuu wa Sweden , STEFAN
LOFVEN amesema hayo alipokutana na
Rais JAKAYA KIKWETE
Ofisini kwake Jijini Stockholm -
Sweden na kuongeza imefika hatua
nyingine ambapo sasa kunahitajika kuanzisha awamu mpya ya uhusiano wa Tanzania
na Sweden.
Kwa upande wake Rais KIKWETE amemwambia Waziri Mkuu wa Sweden
pamoja na misaada ya Sweden kwa Tanzania , awamu nyingine ya uhusiano baina
ya nchini mbili
hizo inahitaji pia kuona
kampuni za Sweden zinawekeza
nchini Tanzania na pia kukuza biashara baina ya nchi mbili hizi ili hatimaye
Tanzania ijitegemee zaidi na kupunguza kutegemea misaada".
Wakati huo huo, Rais mpya ajaye
nchini Tanzania anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha Tanzania
itaendelea kubakia kuwa moja kwa kudumisha Umoja wetu na Amani kwani Tanzania
inatokana na muungano wa nchi mbili.
Rais Jakaya Kikwete ameyasema
hayo j ijini Stockholm - Sweden ali po
kuwa akizungumza na Watanzania wanaoishi
Sweden .
Rais KIKWETE pia ameelezea matumaini yake kuwa
Tanzania itapata kiongozi mzuri na kuelezea mafanikio ambayo serikali yake
imeyapata na kutumaini kuwa yatadumishwa na kuendelezwa na Rais ajaye.
0 comments:
Post a Comment