Kampuni
ya simu za mkononi ya VODACOM nchini kupitia kitengo cha huduma za kijamii
upande wa afya imesema,itaendelea kutoa mchango wake kwa serikali
kwa kuhakikisha afya za akinamama na wasichana zinaboreshwa, na kutokomeza
magonjwa nyemelezi kama FISTULA.
Akizungumza
katika hadhara za uhamasishaji wa wananchi juu ya kutokomeza ugonjwa wa F ISTULA
mkoani Tabora meneja biasharaidara ya mawasiliano Bibi. Grayce Lion
amesema kuwa, kwa kushirikiana na asasi ya CCBRT, kampuni ya VODACOM imetenga
kiasia cha shilingi milioni mia moja kuihamasisha jamii kutokomeza
FISTULA katika mikoa ya Geita, Kigoma na Tabora.
Kwa
upande wake afisa mahusiano wa asasi isiyo ya kiserikali ya CCBRT Bw. Abdul Kajumlo
amesema kuwa, katika jamii bado kuna changamoto ya uelewa juu ya ugonjwa
wa FISTULA, kutokana na baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mahamasisho
yaliyofanyika katika mikoa hiyo.
0 comments:
Post a Comment