Ikiwa na jina Usawa wa Watoto na Fursa ya
Kisheria Ulaya ya Kati na Mashariki pamoja na Asia ya Kati, ripoti hiyo
inaangazia vikwazo dhahiri watoto wanavyokabiliana navyo wakati wakitafuta haki
na suluhisho mujarabu ili kuweka kando ukosefu wa haki na ubaguzi katika maisha
yao.
Hata hivyo inamulika mafanikio katika utawala
wa sheria ikisema kuwa serikali katika ukanda huo zinapiga hatua katika
michakato ya kimahakama ili kulinda haki za watoto kulingana na viwango vya
kimataifa .
Ripoti inasema kuwa msaada wa kisheria na
kijamii kwa watoto katika kuwasadia kupata haki zao unatolewa na kasi
inaongezeka katika huduma hizo kupitia vituo vya haki za watoto au vituo vya
misaada ya kisheria na kupata taarifa kuhusu anuani sahihi za maeneo ya
misaada, kupata ushauri wa kisheria na kupelekwa kwa mwanasheria au mshauri wa
kisaikolojia.
Pia imesema kuwa wakati mwingine watoto
waweza kupata msaada wa kisheria moja kwa moja ilikuanzisha mchakato wa haki.
0 comments:
Post a Comment