Image
Image

Unafahamu kwamba Zabibu hutibu na kutoa kinga ya magonjwa ya ini?''.


Zabibu hujulikana kama chanzo kizuri cha divai, lakini pia huweza kuliwa kama tunda na tunda hili hukuwa katika kichana chenye zabibu 6 hadi 300.

Matunda haya hapa kwetu nchini yanapatikana sana mkoani Dodoma.
Zabibu husaidia kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo.
Matunda haya pia husaidia damu kuwa nyepesi na kuzuia isigande ndani ya mishipa ya damu, hivyo kutokana na sababu hii hupunguza hatari ya kukubwa na kiharusi (stroke)
Zabibu pia inasaidia kuzuia na kutibu tatizo la upungufu wa damu na kwa wale wanaotumia mara kwa mara tunda hili huwasaidia kuepukana na ugonjwa wa bawasili pia.
Hali kadhalika, haya husaidia katika kutibu na kutoa kinga ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.
Mbali na faida hizo, pia zabibu kutokana na kuwa na sukari yake ya asili hivyo huweza kumsaidia mtu katika kupunguza uchovu wa mwili na kutibu maumivu yasiyokuwa na sababu za kueleweka au za moja kwa moja.
Juisi yake husaidia tumbo na utumbo kufanya kazi vizuri na kuzuia ukavu wa haja kubwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment