Siku za hivi karibuni,ukubwa wa tatizo hili umeongezeka, kwani hata vijana wanapatwa na tatizo hili ambalo kitalaam linajulikana kama ‘Gallstones’.
Tunapozungumzia tatizo la mawe kwenye figo siyo mawe halisi, bali huwa ni vitu vinavyojitengeneza kwenye figo taratibu na baada ya muda mrefu hugeuka umbo na kuwa mfano wa vijiwe vidogo vidogo hii hutokana na ulaji wa vyakula usio sahihi.
Mara nyingi tatizo hili hutibika kwa njia ya upasuaji na kuvitoa, huku zoezi hilo likigharimu fedha nyingi na pia husababisha maumivu wakati wa kufanya oparesheni hiyo,Lakini kwa kutumia tiba mbadala ya vyakula, pia huweza kukusaidia kuondokana na tatizo hilo.
Juisi ya tufaa (Pure apple juice) glasi kubwa nne kila siku kwa siku tano mfululizo. Au ulaji wa tufaha nzuri tano badala ya juisi. Tunda hili huweza kusaidia katika kufanya kazi ya kulainisha kwanza mawe tumboni.
Pia unaweza kutumia mchanganyiko wa nusu kikombe cha juisi halisi ya limau na nusu kikombe cha mafuta halisi ya mzaituni (Pure olive Oil). Kinywaji hiki utapaswa kutumia usiku kabla ya kulala.
Pamoja na hayo ni vyema kuweka utaratibu wa kukagua haja yako na utaona vitu rangi ya kijivu au kijani vinavyong’aa na hapo utakuwa umefanikiwa.
0 comments:
Post a Comment