Sam Kutesa ambaye ni Rais wa Baraza hilo
katika hotuba yake amenukuu takwimu ambazo zinaonyesha kuwa kati ya vijana
bilioni Moja nukta Nane duniani kote, Tisa kati ya Kumi wako Afrika ambapo nchi
zao zikiweka mikakati na sera sahihi zinaweza kuwajumuisha kwenye ajira
zitakazobadilisha maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ban Ki-,moon
amesema katika dunia ya leo ambayo vijana Milioni 74 hawana ajira ni tatizo
kubwa kwa hiyo akatoa mapendekezo manne.
"Mosi tuhakikishe huduma za uzazi
wa mpango zinapatikana ili kuepusha magonjwa ya kuambukiza na mimba
zisizohitajika, pili vijana wapate elimu bora na mafunzo na tatu tunahitaji
mafunzo yanayoratibiwa yakizingatia haki za binadamu na utu, na nne hifadhi ya
jamii ya kuondoa umaskini na ukosefu wa usawa."
Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi
waandamizi akiwamo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi na mawaziri kutoka nchi
wanachama wa Umoja huo.
0 comments:
Post a Comment