Kinana, ambaye tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo
amekuwa akikosoa utendaji wa mawaziri na maofisa wengine wa Serikali,
juzi alipokuwa akihitimisha ziara zake mjini Mwanza, alikosoa hata mfumo
wa CCM wa kumfanya Waziri Mkuu kuwa kiongozi wa wabunge.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili
wachambuzi hao walisema kuwa kauli hiyo imechelewa kwa kuwa hakuna
dalili za chama hicho kubadilika kutokana na mifumo, utamaduni na
utawala waliopitia viongozi wengi wa CCM.
Profesa Mpangala: CCM iondolewe
Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha
(Rucu), alisema CCM inatakiwa ifanye vitu viwili ili kuwe na mabadiliko
anayoyataka Kinana.
“Cha kwanza itoke madarakani ili ikajipange upya,
na cha pili kama itabaki madarakani ihakikishe inamchagua kiongozi
shupavu asiyeyumbishwa na mifumo iliyopo ya chama,” alisema Profesa
Mpangala.
Alisema viongozi wa sasa wa CCM wamekuwa
wakituhumiwa kwa rushwa, ufisadi tofauti na siku za nyuma alizosema hata
kama rushwa ilikuwapo ilikuwa kwa kiwango kidogo.
“Chama kimebadilika sana, kimekuwa na viongozi
wabinafsi, wanaotaka maendeleo yao binafsi badala ya wananchi
waliowachagua,” alisema.
“Kauli ya Kinana inaonyesha wazi anataka
mabadiliko na ni wazi kuwa chama hicho kinahitaji mabadiliko ambayo
hayawezi kufikiwa bila kufuata hizo njia mbili. Watoke ili watambue
walikuwa wanakosea wapi kwa kujifunza kwa wenzao watakaoshika dola au
kwa dola nyingine, au wabaki kwa kumuweka kiongozi shupavu asiyeyumba.
“Ninachokiona na kukisema wazi ni kwamba Kinana
hawezi kukibadilisha chama kwa hatua kilichofikia... rushwa, ufisadi,
umimi vimekuwa ndiyo dira. Viongozi wamepoteza mwelekeo, wamejisahau,
wanahitaji muda wa kurekebisha walipokosea.”
Mbunda: Wabunge CCM si makini
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard
Mbunda aliungana na Kinana kukubaliana kuwa wabunge wa CCM si makini na
ndio maana wanapitisha sheria ambazo ni kandamizi kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment