Mwenyekiti wa Kitongoji cha Teya Kata ya Ilindi
wilayani hapa, Paul Mwaja alisema kuwa watoto hao wameuawa katika
matukio mawili ndani ya kipindi cha wiki moja.
Mwaja alisema tukio la kwanza lilitokea juzi
ambapo mtoto mmoja wa kiume mwenye aliuawa na fisi wakati akiwa na
wenzie wawili wamelala. “Alikwenda fisi katika eneo hilo na kumvuta
(mtoto mmoja) na kumtafuna hadi akamuua,”alisema Mwaja.
Alisema usiku wa kuamkia jana, fisi huyo alirudi
tena katika kijiji hicho na kumnyang’anya mama mmoja mtoto wake mdogo
mwenye umri wa miaka miwili.
Mwaja alisema fisi huyo alimla mtoto huyo na kumbakisha kichwa na utumbo tu, hali iliyozua taharuki katika kijiji hicho.
Hata hivyo, alisema baada ya tukio hilo wananchi waliamua kufanya msako na kumkamata fisi huyo na kumuua.
Baba mzazi wa mtoto aliyeuawa usiku wa kuamkia
jana aliyejitambulisha kwa jina moja la Mchamingi, alisema hawana imani
kama fisi huyo kama ni wa kawaida kwani katika tukio la kwanza kabla ya
kuuawa, alikimbilia katika kijiji jirani cha Bahi Makulu na kupotelea
kwenye nyumba za watu.
0 comments:
Post a Comment