Image
Image

watu 10 wamefariki dunia na 134 kulazwa hospitali baada ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu.


Takriban watu 10 wamefariki dunia na wengine 134 kulazwa hospitali baada ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu katika kaunti ya Homa Bay, magharibi mwa Kenya
Mkurugenzi wa huduma za afya wa kaunti hiyo Gerald Akeche amesema, miongoni mwa wagonjwa hao ambao wamelazwa kwenye hospitali za huko ni pamoja na wanawake na watoto. Pia amesema tatizo la vyoo na chakula kinachouzwa mitaani katika sehemu hiyo vimechangia maambukizi ya ugonjwa huo.
Akeche amesema, wakazi wengi wa sehemu za vijijini za Kenya wanapuuza elimu ya msingi ya afya. Kwa mujibu wa wizara ya afya, mwezi uliopita watu 72 walifariki na wengine 3,223 kulazwa hospitali kutokana na ugonjwa wa kipindupindu.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment