Watu 28 wamekufa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa baada ya bomu lililokuwa kwenye gari kulipuka jirani na hospitali ya jeshi katika Mji Mkuu wa Yemen, Sanaa .
Katika taarifa iliyowekwa kwenye mtndao kikundi
cha Islamic State cha Iraq
kimedai kuhusika na shambulio hilo la bomu na kuongeza kuwa kimeandaa
shambulio ilichosema dhidi ya Kiota cha
Washia kwenye Mji wa Sanaa.
Bomu hilo liliwalenga ndugu
wawili wa kiongozi wa waasi wa Houthi,
ambao ni FAY SALna HAMID JAYACHE kwenye
mkusanyiko wa maziko ya mwanafmilia wao mmoja.
Muungano wa kijeshi unaoongozwa
na Saudi Arabia umekuwa ukishambulia kwa mabomu maeneo
yanayaokaliwa na Wahouthi wengi
Mjini Sanaa kwa lengo la kutaka kumrejesha Rais wa Yemen aliye uhamishoni nchini Saudi Arabia Bwana ABD-RABBU MANSOUR
HADI.
0 comments:
Post a Comment