Watu 30 wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya ndege
ya mizigo ya jeshi la Indonesia kuanguka kwenye makazi ya watu katika Mji wa Medan nchini humo.
Televisheni ya Indonesia
imeripoti kuwa ndege hiyo imeangukia
kwenye nyumba mbili na gari na
kisha kuwaka moto.
Msemaji wa Jeshi la Indonesia,FUAD
BASYA amewaambia Waandishi wa Habari
kuwa ndege hiyo imeanguka muda mfupi baada ya kuruka na ilikuwa na wafanyakazi
12.
Msako mkubwa unaendeshwa kwenye
eneo ndege hiyo ilipoanguka ambayo
limekumbwa na miali ya moto na moshi mzito.
Waandishi wa Habari wanasema hii ni
maraya pili katika kipindi cha miaka kumi, ndege kuanguka kwenye vitongoji vya
Mji wa Medan.
Septemb a 2005, ndege aina ya Boeing 737 ilianguka kwenye makazi ya watu muda mfupi baada ya kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Polonia na kusababisha vifo vya watu 143 ,wakiwemo 30 waliokuwa ardhini.
0 comments:
Post a Comment