Image
Image

Watu zaidi ya 800 waarifiwa kufariki dunia kutokana na joto kali Kusini mwa Pakistan.



Idadi  ya watu waliokufa kutokana na wimbi la joto kali Kusini mwa Pakistan ni zaidi ya watu 800.

Habari zinasema kuna uwezekano wa idadi hiyo kuongezeka kutokana na hali ya joto kali kuendelea  kwa siku ya nne leo.

Dakta  SEEMIN JAMALI   wa Hospitali ya Jinnah ambayo ni hospitali kubwa zaidi Mjini Karachi amesema, vyumba vya kuhifadhia maiti vimelewa na wingi wa maiti.

Amesema tangu  Jumamosi iliyopita hospitali hiyo ya Jinnah imepokea wagonjwa 800 walioathirika na hali ya wimbi la joto kali na kati yao wagonjwa 384 wamekufa.

Mmoja wa wafanyakazi wa afya wa kujitolea,  JUNAID AHMAD   amesema watu wengi wanaofikishwa hospitali ni wenye umri wa kuanzia miaka 45 hadi 50.




Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment