Uhaba wa huduma za
kutosha za majisafi na kujisafi uliibua changamoto na mlipuko kuripotiwa
miongoni mwa wakimbizi hasa kwenye kijiji cha Kagunga kilichoko mpakani, halikadhalika
kambini Nyarugusu.
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na shirika la afya
duniani, WHO walihaha kutwa kucha kudhibiti mlipuko huo uliosababisha vifo vya
watu 30 na wengine zaidi ya 4,400 kuambukizwa.
Jitihada hizo ni pamoja na
kutuma wataalamu wa afya wakiwemo wanasayansi wa maabara miongoni mwao Jacob
Lusekelo, mwanasayansi wa maabara kutoka Maabara kuu ya Taifa nchini Tanzania.
Akihojiwa kwa njia ya simu kutoka Tanzania na Assumpta Massoi wa Idhaa
hii, Bwana Lusekelo anaelezea kile walichofanya na jinsi huduma yao
ilivyosaidia kudhibiti mlipuko. Kwanza anaelezea hali ilivyokuwa walivyowasili
Kigoma.
0 comments:
Post a Comment