Baada ya msanii kutoka Ghana Fuse ODG kuwachana waandaji wa Bet kwa
kutoa tuzo za wasanii wa Afrika mapema kabla ya show na eneo
wanalopokelea tuzokuwa ni back stage, msanii mwingine mkubwa wa Nigeria
‘Wiz Kid’ pia amefanya hivyo.
Kupitia kurasa yake ya twitter Wiz anasema hakuhudhuria tuzo hizo
zilizofanyika jumapili ya tarehe 28 June sababu hakuona maana kama
angepata tuzo angeipokea saa nne asubuhi kabla ya show, Wiz anaendelea
kusema kuwa hana imani na tuzo sababu ni watu wamekuja pamoja
kutayarishwa show yao tu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment