Mabao ya Argentina yalifungwa na winga wa Manchester United,
Angel di Maria aliyefunga mawili na huku Marcos Rojo, Sergio Aguero, Javier
Pastore na Gonzalo Higuain wakifunga bao moja moja kila mmoja.
Beki wa Manchester United, Marcos Rojo alianza kuifungia
Argentina dakika ya 15, kabla ya Javier Pastore kufunga la pili dakika ya 27 na
Lucas Barrios kuwafungia bao la kufutia machozi Paraguay kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili Angel di Maria akaanza ‘balaa lake’
akiifungia Argentina bao la tatu na la nne dakika ya 47 na 53, kabla ya Sergio
Aguero kufunga la tano dakika ya 80 na Gonzalo Higuain la sita dakika ya 83.
Argentina watapambana na Chile July 04 kwenye uwanja wa
taifa uliopo mjini Santiago na siku moja kabl ya mchezo huo Peru watapambana na
Paraguay katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu.
0 comments:
Post a Comment