Kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike imezindua rasmi mipira
itakayotumika kwenye ligi za nchini England, Italia pamoja na Hispania kwa
msimu wa 2015-16.
Kampuni ya Nike inayodhamini ligi hizo upande wa vifaa,
imezindua mipira hiyo kwa kutoa picha ambazo zinaonyesha utofauti uliopo kwa
kuzingatia rangi ambazo zitatumika.
Ligi ya nchini Englnd ambayo ni maarufu sana duniani
itatumia mpira ulionakshiwa rangi ya nyekundu kwa kiasi kikubwa na ligi ya
nchini Hispania utatumia mpira wenye asilimia kubwa ya rangi ya pink huku ligi
ya nchini Italia itakuwa na mpira ulionakshiwa rangi ya kijani mpauko.
Hata hivyo mipira hiyo mitatu imetengeneza kwa malighafi
moja na kinachoitofautisha ni rangi.
0 comments:
Post a Comment