Nature kurekodi nyimbo zake kali zilizowahi kuvuma kipindi cha miaka ya nyuma.
Juma Kassim Kiroboto a/k/a Nature, Msanii Mkongwe wa muziki wa Bongo Flava nchini amesema mwaka huu ataanza utaratibu wa kurudia kurekodi nyimbo zake kali zilizowahi kuvuma kipindi cha miaka ya nyuma. Akizungumza kupitia kipindi cha Bongo.Home kinachoruka hewani kila siku za Jumamosi saa 10:00 mpaka 12:00 jioni ndani ya Radio Times Fm, Juma Nature amesema ameamua kufanya hivyo baada ya kuombwa na mashabiki wake arudie baadhi ya nyimbo zake.
“Baada ya mwezi huu mtukufu wa ramadhani nitaanza kurekodi nyimbo zangu, ambazo mashabi wamezichagua kwa kuwa wanazipenda sana”, alisema Nature.
Nature amezitaja nyimbo hizo kuwa ni Inaniuma Sana, Sitaki Demu na Sonia.
0 comments:
Post a Comment