Kocha msaidizi wa klabu ya Simba Suleyman Matola amesema
mipango ya kusajiliwa kwa Kiiza ilipendekezwa na benchi lao la ufundi kufuatia
hitaji mshambuliaji ambalo anaamini limepatiwa ufumbuzi, baada ya kuonekana
ulikua na mapungufu msimu uliopita.
Matola amesema ujio wa Mshambuliaji huyo ambaye alitemwa na
klabu ya Dar es salaam Young Africans wakati wa dirisha dogo la usajili
mwishoni mwa mwaka 2014, utaongeza chachu kwa wachezaji wenzake ambao tayari
wameshaanza mazoezi ya Gym.
“Kama tasajiliwa Kiiza itakua ni vizuri sana kwetu, kwa
sababu sisi tulipendekeza usajili wa mchezajia nayecheza nafasi ya ushambuliaji
baada ya kuona mapungufu msimu uliopita.” Alisema Matola
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya
Simba, Zacharia Hans Poppe amesema wako katika hatua za mwisho kumsajili
mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Hamis Kiiza.
Kwa upande wa mshambuliaji huyo ambaye alikua mpambe wa
bwana harusi wakati wa sherehe ya ndoa ya Emmanuel Okwi mwishoni mwa juma
lililopita, amesema wakala wake amefikia hatua nzuri na Simba, hivyo wakati
wowote anaweza kusaini mkataba.
“Ni kweli wakala wangu amekuwa akizungumza na Simba,
ameniambia wamefikia hatua nzuri, wakimalizana kila kitu, nitasaini Simba”.
Amesema Kiiza.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga amesema kama atajiunga
na Simba itakuwa furaha kwake kucheza timu moja na rafiki yake Emmanuel Okwi.
“Okwi ni rafiki yangu wa siku nyingi toka tukiwa shule,
tulicheza pamoja toka tukiwa wadogo, ndio maana uliona hata kwenye harusi yake
mimi nilikuwa msindikizaji wake, nitafurahi kucheza naye Simba”. Ameongeza
Kiiza.
0 comments:
Post a Comment