Msemaji wa Wa-Houthi Bwana ALI
AL-AHMADI amesema wapiganaji hao pamoja
na washirika wao wamerusha makombora 15
kwa wanajeshi watiifu kwa Serikali
ya Yemen kwenye maeneo ya Dar Saad.
Shambulio hilo limekuj baada ya
bomu lililokuwa kwenye gari kuwalenga
viongozi wa Houthi katika Mji mkuu wa
Yemen - Sanaa, na kikundi cha Islamic State
cha Iraq kudai kuwa kimehusika na shambulio hilo juzi na kusababisha
vifo vya watu 28.
Wakati huo huo, wakati
mapigano yanaendelea, Maafisa wa Yemen wanasema wafungwa 1,200, wakiwemo
watuhumiwa wa kikundi cha ugaidi cha al-Qaeda wametoroka kwenye gereza moja
kwenye Mji wa Taiz, katikati ya Yemen.
0 comments:
Post a Comment