Baadhi ya bei za bidhaa katika soko la kariakoo jijini DSM,
zimeshuka kutokana na kipindi cha msimu wa mavuno ya mazao hayo kuanza
ambapo Mtakwimu wa shirika la masoko la kariakoo HENRY RWEJUNA amezitaja
bidhaa hizo kuwa ni nyanya, njegere na vitunguu maji
RWEJUNA ameeleza kuwa hivi sasa kasha la kilo 40 la nyanya linauzwa kwa kati ya shilingi elfu 15 na elfu 20 ambapo hapo awali liliuzwa kwa kati ya shilingi elfu 30 na shilingi elfu 40.
Gunia la kilo la vitunguu maji linauzwa kwa shilingi 150,000 na shilingi 160,000 ambapo awali liliuzwa kwa kati ya shilingi 250,000 na shilingi 280,000.
Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara sokoni hapo wamesema baadhi ya bidhaa zimepanda bei kutokana na kuwa si msimu wake

0 comments:
Post a Comment