Image
Image

Mapigano Somalia yasababisha vifo vya watu 35.

Mapigano kati ya kundi la kigaidi la al-Shabab na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) yamesababisha vifo vya watu 32.
Habari zinasema kuwa, wanajeshi wa AMISOM wakishirikiana na jeshi la Somalia wamekabiliana vikali na al-Shabab tangu jana ambapo magaidi 25 wameuawa. Duru rasmi kutoka AMISOM pia zinasema kuwa wanajeshi 7 wa Somalia na raia wawili wamepoteza maisha kwenye makabiliano hayo.
Tangu kufurushwa kutoka mji mkuu wa Somalia, Mogadishu mwaka 2011, kundi la al-Shabab lilikimbilia kusini mwa nchi hiyo na kushikilia miji kadhaa. Hata hivyo, tangu kuanza mwaka huu wa 2015, kundi hilo la kigaidi na kitakfiri limepata pigo kwa kupoteza udhibiti wa takriban asilimia 80 ya miji iliyokuwa chini yake baada ya kuzidiwa nguvu na majeshi ya Somalia yakisaidiwa na AMISOM.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment