Akizungumza na wakazi wa
Wilaya ya Urambo katika mkutano wa hadhara, Mkurugenzi wa Ulinzi na
usalama wa CHADEMA , WILFRED LWAKATARE amesema
wataendelea kuwaeleza
ukweli wananchi hatua ambayo itasaidia kuwafumbua macho kuhusu wimbi la wanaosaka madaraka hasa
kupitia Chama cha Mapinduzi
kuwa hawana ukweli wa
kuwasaidia wananchi.
Katika hatua nyingine wakati
akifunga mafunzo ya vijana Red Brigedi
wa CHADEMA wapatao
mianane wilayani Urambo Mkurugenzi
huyo wa Ulinzi na Usalama
amewataka vijana hao
kuwa makini na baadhi ya
wanasiasa wanaotaka kuwatumia wakati
huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.


0 comments:
Post a Comment