Ulaji wa matango na matikiti maji husaidia kuboresha kiwango cha maji
ambayo huitajika mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango
kikubwa cha maji ambayo husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu
mbalimbali ambazo miili yetu huzipata kupitia vyakula, madawa na hata
vinywaji.
(1)Husaidia kupunguza uzito wa mwili. Kutokana na kuwa
na asili ya nyuzi nyuzi au, fibres, humfanya mlaji ajisikie kushiba bila
ya kuongeza vitu mwilini ambavyo husababisha mtu aongezeke uzito hivyo
kuzuia magonjwa mbalimbali
(2)Hupunguza (hangovers),uchovu,
mawengewenge pamoja na hali ya kujisikia vibaya kutokana na unywaji wa
kilevi. Hii ni kutokana na kuwa na vitamini B na maji mengi ambapo,
baada ya mtu kunywa kilevi na kisha akaja kula matango kabla ya kulala,
itamfanya asubuhi asiamke huku akiwa na hangovers
(3)Husaidia
katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya tumbo kama vile kuvimbiwa,
tumbo kujaa gesi, vidonda vya tumbo na mengineyo hupungua kutokana na
ulaji wa matango, husaidia kuondoa sumu tumboni na kurahisisha
ufyonzwaji wa protein mwilini kutokana na uwepo wa kiwezeshaji cha
kibaiolojia kinachoitwa, erepsin enzyme.
(4)Husaidia kuondoa
msongo wa mawazo kwani yana kiwango kikubwa cha vitamini B ambayo
husaidia kuboresha utendaji kazi wa mishipa mbalimbali ya fahamu mwilini
na hivyo kuondoa hatari ya mtu kuathirika na msongo wa mawazo
unaosababishwa na maisha ya kila siku.
(5)Husaidia
kuondoa hatari ya mtu kupata kansa. Yana kiwango kikubwa cha virutubisho
vyenye asili ya mimea viitwavyo, lignans, ambavyo pamoja na vitamini
c,
(6)husaidia kuondoa sumu mbalimbali na kuiboresha kinga ya mwili na hivyo kuepusha hatari ya mtu kupata kansa.
(7)Husaidia
kuondoa harufu mbaya kinywani. Kwa kukiweka kipande cha tango mdomoni
kwa dakika kadhaa, huuwa bakteria mbalimbali wasababishao magonjwa
mbalimbali ya kinywa na harufu mbaya mdomoni.
(8)Husaidia mtu kupata choo laini na huzuia kukosa choo.
(9)Huzuia
kuganda kwa mafuta katika mishipa ya damu ili kuwezesha mzunguko sahihi
wa damu kaitika pande zote za mwili sambamba na kurekebisha mapigo ya
moyo
(10)Huwepo wa vitamini katika matunda haya husaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini na presha.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment