Miongoni mwa makada waliorudisha fomu hizo ni pamoja na waziri mkuu mstaafu Mhe Edward Lowassa ambaye ameambatana na maelfu ya wafuasi na kufanya viwanja vya makao makuu ya ccm kufurika watu ambapo amesema ana shauku kubwa ya kuunganisha nguvu na uwezo wa kila mtanzania katika kupambana na umasikini kwani umasikini kamwe sio amri ya mwenyezi mungu.
Kada mwingine ni naibu
waziri wa fedha mhe Mwigulu Nchemba ambaye pamoja na mambo mengine amesema
endapo atapewa ridhaa na wana cch na kisha watanzania wakamchagua kuwa kiongozi
wao atahakikisha anakabiliana na rushwa iliyokithiri na kutatua tatizo sugu la
ajira hasa kwa vijana kwa kuongeza fursa za ajira na uwekezaji.

Lazaro Nyalandu waziri wa utalii ambaye na yeye amejitosa katika kinyang'anyiro hicho naye pia amerudisha fomu akiomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania urais huku ambaye pamoja na mambo mengine ameahidi kuinua uchumi wa nchi utakaotegemea rasilimali zilizoko nchini kwa manufaa ya wate.
Dk Hass Kitine mkurugenzi wa zamani wa idara ya usalama wa taifa ni miongni mwa makada waliotupa turufu yao kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi kupitia ccm huku akitilia msisitizo suala la utawala bora unaozingatia miiko na maadili ya uongozi akiwa na imani kuwa mambo hayo ndio msingi wa maendeleo wa taifa lolote lile duniani lililopiga hatua kiuchumi.
makada wengine waliojitokeza hii leo ni pamoja na Dk .Hamis Kigwangala mbunge wa nzega ambaye amesema imefika wakati sasa taifa kupunguza mamlaka za uteuzi hasa katika nafasi ya urais ili kuongeza uwajibikaji huku idadi kamili ya waliorudisha fomu hadi hvi sasa ikiwa ni kati ya makada 41 waliojitokeza.



0 comments:
Post a Comment