Wamesema maabara zinazojengwa kwa
agizo la Rais JAKAYA KIKWETE halitakidhi haja na vigezo muhimu kutokana na
ukosefu wa walimu, hali itakayoifanya
Tanzania kushindwa kufanya mabadiliko ya teknolojia na kusababisha taifa
kushindwa kuingia katika soko la ushindani wa ajira duniani.
Hayo yamesemwa na wanafunzi wa masomo ya sayansi katika shule za
sekondari Old Shinyanga, Mazinge, Ngokolo na Kizumbi wakati wa hafla ya kupokea
maabara nne zilizojengwa na kampuni ya ACACIA inayomiliki mgodi wa dhahabu wa
Buzwagi.
Kwa upande wake meneja wa kampuni
ya ACACIA Buzwagi Bwana PHILBERT ROYMAM amesema lengo la kampuni yake ni
kuhakikisha maabara hizo zinakuwa chachu ya kupatikana wataalamu wa uhakika
watakaoweza kuleta maendeleo.


0 comments:
Post a Comment