Wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro
wenye matatizo ya macho wamejitokeza kwa wingi katika hospitali ya rufaa ya
mkoa huo MAWENZI - kupata huduma ya matibabu na upasuaji wa mtoto wa jicho
inayotolewa na madaktari bingwa kutoka Ubelgiji bila ya malipo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
huduma hiyo inayofadhiliwa na Lions Club,
MRAtibu wa Lions Club ya Kibo Kilimanjaro, Bwana NITU REHAL amesema madaktari hao bingwa
watatoa huduma bure kwa watu wote wenye
matatizo ya macho katika Wilaya za Moshi, Hai na Siha na watoto wenye albinism.
Amesema madaktari hao wanatoa
huduma hiyo kwa kushirikiana na madkari wa macho Mkoani Kilimanjaro kwa siku
kumi na kwamba ni vema wananchi wenye matatizo ya macho hasa ususani maeneo ya
vijijini kujitokeza kupatiwa vipimo, matibabu na wale wenye tatizo la kuchunwa
na kufanyiwa upasuaji.
Kwa upande wake Raisi wa
Madaktari bingwa wa macho kutoka Shirika la See and Smile nchini Ubelgiji, Dakta
CLAEYS MARNIX amesema kwa siku wanahudumia watu 250 na kwamba mpaka sasa
wengi waliofanyiwa vipimo wamebainika kuwa na tatizo la mto wa jicho pamoja na
trakoma.


0 comments:
Post a Comment