Image
Image

Miili 141imepatikana baada ya ndege ya mizigo ya jeshi la nchi hiyo iliyoanguka Mjini Medan.


Maafisa wa Serikali ya Indonesia wamesema  miili 141imepatikana baada ya ndege ya mizigo ya jeshi la nchi hiyo iliyoanguka jana kwenye makazi ya watu Mjini Medan.
Afisa mmoja wa Polisi,AGUSTINUS TARIGAN amewaambia Waandishi wa Habari leo asubuhi kuwa miili ya watu 141 imepatikana kutoka eneo ilikoanguka ndege hiyo.

Jeshi la nchi hiyo limesema hakuna mtu aliyenusurika miongoni mwa watu 122 waliokuwemo kwenye  ndege hiyo Hercules C-130, ilipogonga nyumba na   hoteli na kisha kuwaka moto.

Taarifa imesema wengi wa watu waliokfua  inaaminika kuwa ndugu wa wanajeshi na taarifa za hivi karibuni zinasema watu 19 wamekufa ardhini ambako ndege hiyo imenguka.

Chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo hakijajulikana, lakini walioshuhudia tukio hilo wanasema inaeleke ilikumbwa na tatizo muda mfupi baada kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Mji wa Medan, ambao ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Indonesia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment