Image
Image

Kiiza awekewa masharti Simba.

UONGOZI wa Simba umesema mchezaji wa zamani wa Yanga, Hamis Kiiza atajiunga na klabu hiyo kwenye mazoezi kati ya leo au kesho iwapo tu atafuzu vipimo vya afya.
Kiiza, ambaye alitemwa Yanga msimu uliopita, alitarajiwa kuwasili wakati wowote kuanzia jana, na leo atapimwa afya ili kuungana na wachezaji wengine wa Simba katika mazoezi.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari jana, Rais wa Simba Evans Aveva alisema Kiiza atakuwa mchezaji halali wa Simba iwapo atafuzu vipimo leo.
“Kiiza atatua muda wowote kuanzia leo (jana) na akifaulu vipimo vya afya moja kwa moja atakuwa mchezaji wetu,”alisema.
Mchezaji huyo Mganda alitemwa na aliyekuwa Kocha wa Yanga, Mbrazili Marcio Maximo msimu uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na Kpah Sherman. Kiiza hivi karibuni alinukuliwa kwenye vyombo vya habari akithibitisha ujio wake wa kujiunga na Simba.
Iwapo atafanikiwa kusajiliwa Simba atatimiza jumla ya wachezaji wanne wanaotoka Uganda baada ya Emmanuel Okwi na Simon Sserunkuma na Juuko Murshid huku Raphael Kiongera akitokea Kenya.
Katika hatua nyingine, Aveva alisema atatangaza rasmi kambi ya maandalizi ya msimu kabla ya kumalizika kwa wiki hii.
Alisema kocha mpya wa mazoezi ya viungo, Dusan Momcilovic na makipa Abdul Salim wataungana na kikosi cha Simba leo kwenye mazoezi kuanza kazi rasmi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment