Pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mh James Mbatia, Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe, Waziri mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa na Mwenyekiti wa CUF Prf Ibrahimu Lipumba.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya kujiunga na CHADEMA Waziri mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa.
Mh Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya Kujiunga na CHADEMA mama Regina Lowassa.
Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa na Mkewe mama Regina Lowassa wakionyesha kadi zao za Uanachama wa CHADEAMA mara baada ya kujiunga na CHADEMA katika hafla iliyofanyika Bahari Beach Hotel.
Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa akiwa na Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Lipumba
Mwenyekiti wa Baraza la wanawake CHADEMA na Mbunge wa Kawe Mh Halima Mdee akisikiliza kwa makini yaliyokuwa yakijili katika hafla ya kujiunga na Chadema kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh Edward Lowassa.
Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Mheshimiwa EDWARD LOWASSA a mesema ameamua kukihama Chama Cha Mapinduzi na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, baada ya kutafakari kwa kina yaliyotokea katika mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Mheshimiwa LOWASSA amesema hayo jijini
Dar es salaam katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Demokrasia na
Maendeleo-CHADEMA kwa niaba ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi-UKAWA kumpokea kama wanachama mpya wa CHADEMA.
Amesema mchakato wa kuteua wagombea
ulighubikwa na mizengwe , ukiukaji wa maadili, uvunjaji wa katiba na taratibu
za uchaguzi ndani ya CCM.
Aidha,amesema uchaguzi ulisimamiwa kwa
upendeleo na chuki iliyokithiri dhidi yake.
Amesema kikatiba ya Chama Cha Mapinduzi,
Kamati ya maadili siyo chombo rasmi na haina madaraka ya kuchuja na kupendekeza
majina miongoni mwawale wanaoomba kugombea urais kupitia CCM.
Amesema kilichotokea Dodoma ni kupora
madaraka ya Kamati Kuu na kuikiuka katiba ya CCM.
Mheshimiwa LOWASSA Kamati Kuu ya
Halmashauri kuu iliitishwa na kuburuzwa ili ielekeze azma ya watu binafsi
pasipo kujali demokrasia, katiba. Kanuni na taratibu za uchaguzi ndani ya CCM.
Wakati huo huo idadi kubwa ya wanachama
wa Chama ChaMapinduzi katika halmashauri ya Ushetu wilayani wamehamia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kwa madai kuwa wamechukizwa na kile
wanachokiita fitina zinazoendelea katika Chama Cha Mapinduzi.
Aidha, wamesema wamefanya hivyo kumuunga
mkono mbunge wao JAMES LEMBELI katika harakati za ukombozi wa kweli kwa
wananchi pamoja na wakulima wa tumbaku na pamba wanaodhulumiwa kila kukicha.
Matukio hayo yametokea kwa nyakati
tofauti katika mikutano ya aliyekuwa mbunge wa Kahama kwa tiketi ya CCM
Mheshimiwa JAMES LEMBELI ambaye amehamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
-CHADEMA
Katika hali isiyotarajiwa mke wa
mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu
JUMANNE KIMISHA, JUSTINE KIMISHA
amechukua fomu ya kugombea udiwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
-CHADEMA pamoja na mumewe anayegombea kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Amesema aliwekwa mizengwe na kuzushiwa
majungu na uongo mwingi kuhakikisha kuwa jina lake halifikshwi mbele ya Kamati
Kuu na Halmashauri Kuu kujadiliwa, licha ya ukweli usiopingika kuwa alikuwa
mgombea aliyeungwa mkono na wanachama na wananchi wengi zaidi kuliko wenzake
wote.
Amesema kibaya zaidi ni kile kitendo cha
kuwanyima wagombea 38 haki ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu.
Amesema kwa kifupi anaamnini kuwa
hakutendewa haki katika mchakato mzima wa kupendekeza majina na kuteua mgombea
urais kupitia CCM.
Amesema baada ya kutafakari kwa kina
ameamua kuwa kuanzia leo anaondoka CCM na kuitikia wito wa UKAWA kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA kuungana nao katika kuleta mabadiliko ya
kweli kwa nchi.
Wakizungumza katika mkutano huo,
viongozi wakuu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA
wamempongeza Mheshimiwa LOWASSA na kumuahidi kumpa ushirikiano katika azma yao
ya kuwaletea wananchi maendeleo.
0 comments:
Post a Comment