Matokea ya uchaguzi Burundi yatarajiwa kabla ya Alkhamisi.
Kura zimeanza kuhesabiwa punde tu baada ya kumalizika kwa mudu ulioweka wa kupiga kura nchini kote Burundi.
Uchaguzi wa rais umefanyika katika usalama licha ya ghasia zilizodumu kwa muda wa miezi miwili nchini Burundi.
Vyama vya upinzani na asasi za kiraia vilitoa wito wa maandamano dhidi ya muhula wa 3 wa rais Nkurunziza kwa kufahamisha kuwa muhula wa 3 wa rais Nkurunziza ni kinyume na katika ya Burundi.
Tume iliyosimamia uchaguzi imefahamisha kuwa uchaguzi umekwenda vizuri kama ilivyotarajiwa.
0 comments:
Post a Comment