Image
Image

Mrahaba wa madini uwanufaishe wajasiria mali Mererani.


Shughuli ya kuchimba na kutafuta madini aina ya Tanzanite yanayopatikana katika mgodi wa Mererani mkoani Arusha ikiendelea. Picha na Maktaba.
Wajasiriamali wadogo katika mji wa Mererani Wilayani Simanjiro wameiomba Serikali itoe sehemu ya pato inalokusanya kutoka kwenye kodi inayotokana na madini ya Tanzanite na kuvipa  vikundi vya  wajasiriamali ili wanufaike na rasilimali inayowazunguka ili  wajikwamue na hali ngumu ya umasikini.

Wakizungumza katika uzinduzi wa vikundi vya wajasirimali wadogo wanawake wajasiriamali katika mji wa Mererani wamesema wamekuwa na juhudi za kujiunga katika vikundi vya Vikoba na vinginevyo ili kujikwamua kiuchumi lakini juhudi zao zinagonga mwamba kwa kukosa mitaji.

Wamedai kuwa hali hiyo inatokana na Serikali kutochangia juhudi hizo wakati wanaishi katika mji wenye rasilimali muhimu ya madini ya Tanzanite hivyo wameiomba serikali itoe sehemu ya pato la madini hayo kuunga mkono juhudi zao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment