Mtu aliyefahamika kwa jina la selemani maporomoko ameuawa kinyama na jirani yake aliyefahamika kwa jina la Mohamed Wajisiku baada ya kuwa na mgogoro wa muda mrefu wa kugombea eneo la shamba lenye heka moja na nusu katika kijiji cha malanje kata ya ntiniko wilaya ya mtwara vijijini.
**Huu ndio mwili marehemu ukiwa umelala pembezoni mwa barabara kuu ya wilaya ya mtwara vijijini
na tandaimba.**
Akithibitisha tukio hilo kwa njia ya simu
kamanda wa polisi mkoa wa mtwara Henrry Mwaibande amesema marehemu alikutwa na
tukio hilo majira ya alfajiri wakati akisafirisha biashara yake ya mbao kwenda
mjini kwa baiskeli na ndipo alipoviziwa na jirani yake na kumshambulia kwa
mapanga sehemu mbali mbali za mwili na hatimaye kupoteza maisha.
**Iliyoko Chini hapo ni baiskeli
iliyokuwa imefungwa mbao,ndala za marehemu na kofia,na hawa ni mashuhuda wa
tukio hilo.**
Kwa
mujibu wa kamanda mtuhumiwa ametoroka na baiskeli yake ilikutwa eneo la tukio
hali iliyowapandisha asira wananchi na kuamua kwenda nyumbani kwake
na baada ya kumkosa waliamua kuvunja nyumba kubeba kila kitu na hatimaye
kuichoma nyumba hiyo moto.
0 comments:
Post a Comment