Image
Image

Ngoma aahidi makubwa Yanga.

MS H A M B U L I A J I mpya wa Yanga, Mzimbabwe Donald Ngoma, amewataka mashabiki wa timu hiyo kusubiri mambo mazuri kutoka kwake ikiwa ni muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo.
Ngoma aliyetambulishwa rasmi jana kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga sambamba na beki Mghana Joseph Zuttah, alisema amejipanga kufanya kazi kubwa na kuipa mafanikio timu hiyo ili aweze kudumu kwa muda mrefu kama ilivyokuwa FC Platinum.
“Najisikia furaha kucheza Yanga kwa sababu ni klabu kubwa Tanzania nitahakikisha natumia uwezo wangu, naongeza mafanikio yaliyopo kwa kushirikiana na wenzangu niliowakuta,”alisema Ngoma.
Kwa upande wake, Zuttah alisema ametua Yanga kwa kazi moja tu ya kuendeleza mazuri yaliyofanywa siku za nyuma na amekuja akiwa kamili na kuwataka washabiki wa timu hiyo kumpa sapoti.
“Nimefurahi kuona mashabiki wanaipenda sana timu yao kuanzia Jumamosi wakati Yanga ilipocheza na Sports Club Villa nimehamasika sana kitu ambacho kimenifanya nisijutie maamuzi yangu ya kucheza Tanzania,”alisema Zuttah.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro wachezaji hao wameshamalizana nao kila kitu na tayari wameshawasilisha usajili wao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ili waweze kuombewa kibali cha kufanyia kazi.
Ngoma ametua Yanga aki tokea FC Platinum ya Zimbabwe wakati Zuttah alikuwa akikipiga klabu ya Medeama ambao ni mabingwa wa Kombe la FA nchini Ghana.
Baada ya kuwanasa wachezaji hao wawili, tayari Yanga imekamilisha idadi ya nyota saba wa kimataifa inayotakiwa kwa mujibu wa kanuni za TFF, ambapo wengine ni Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Andrey Coutinho na Mbuyu Twite.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment