Image
Image

Polisi wakabiliana na waandamanaji waliokuwa wakipinga uamuzi wa serikali nchini Ugiriki.


Maandamano ya kupinga uamuzi wa kuiokoa nchi uliokubaliwa na serikali yalifanyika katika mji mkuu wa Athens nchini Ugiriki.
Takriban watu elfu moja waliokusanyika katika eneo la wazi la Sintagma nyakati za jioni, waliandamana kupinga uamuzi huo uliokubaliwa na serikali ya Ugiriki.
Polisi walitumia mabomu ya machozi ili kukabiliana na waandamanaji waliokuwa wakiwarushia vilipuzi vya chupa.
Baada ya makabiliano ya polisi, baadhi ya waandamanaji walitorokea mitaani na kundi moja la watu likachoma moto gari la kupeperusha matangazo ya moja kwa moja linalomilikiwa na kituo cha televisheni cha Antenna nchini Ugiriki.
Polisi walifunga njia barabara zote na kushika doria katika jengo la bunge lililokuwa karibu na Sintagma.
Takriban waandamanaji 50 wameirpotiwa kutiwa mbaroni na polisi katika tukio hilo.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment