Image
Image

Uchaguzi wafanyika katika hali tete nchini Burundi.


Takriban watu milioni 3.8 ndio waliojirodhesha kupiga kura katika uchaguzi wa rais nchini Burundi unaoripotiwa kuanza kufanyika leo nchini kote Burundi.
Uchaguzi huo unafanyika ikiwa wagombea kutoka katika vyama vya upinzani walifahamisha kususia uchaguzi kwa kusema kuwa hautokuwa wa haki.
Uchaguzi unafanyika katika hali tete baada ya kusitishwa kwa mazungumzo baina ya serikali na upinzani yaliokuwa yakiongozwa na waziri wa ulinzi wa Uganda.
Upinzani na asasi za kiraia walitowa wito wa maandamano dhidi ya muhula wa 3 wa rais Nkurunziza.
Marais wa zamani wa Burundi, Domitien Ndayizeye, Sylvestre Ntibantunganya na Jean Minani ambao walikuwa wagombea kiti cha urais walifahamisha kuwa majina yao katika matokeo ya uchaguzi hayano umuhimu wowote ule.
Tume ya uchaguzi CENI ilifahamisha kuwa wagombea hao hawakujitoa katika uchaguzi wakiheshimu taratibu zilizowekwa na tume hiyo.
Kwa mujibu wa serikali, wangomea wanane ndio wanaowania kiti cha urais katika uchaguzi huo.
Jijini Bujumbura kumeripotiwa milio ya risasi usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne na kusababisha askari mmoja na raia mmoja kufariki.
Msemaji wa rais, Willy Nyamitwe amefahamisha katika akaunti yake ya Twitter kuwa mashambulizi hayo ya kigaidi yalikuwa na nia ya kuwatisha watu wasijielekezi katika vituo vya kupigia kura.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment