Moja ya utalii mbadala ambao umejitokeza na kushamiri sana katika
dunia ya leo ni utalii wa kiafya. Idadi ya watu ambao husafiri kutoka
nchi moja na kwenda katika nchi nyingine ili kupata matibabu ya kiafya
imekua kubwa mno.
Katika uhusiano na hili, ukubwa wa soko la utalii
kupitia sekta ya afya umeongezeka mara dufu na kufikia kiasi cha dola
milioni 100.
Kuna sababu kemkem zinazosababisha kuboreka na kuimarika kwa sekta
hii duniani kote. Moja ya sababu kubwa kabisa ni kuwa serikali nyingi
duniani huondosha magonjwa ya kiasthetiki, magonjwa ya meno na
upandikizaji nywele katika orodha ya mfuko wa ulinzi wa jamii. Sababu
nyingine ni kipindi cha kusubiri tiba. Operesheni zinazofanywa katika
nchi nyingi kama Canada au Uingereza huwa na muda mrefu wa kusubiri
takriban mwaka mmoja na nudsu hadi miwili.
Lakini sababu kuu kabisa na ya msingi ni unafuu wa gharama za
matibabu. Upasuaji ambao hufanywa kwatakriban dola laki moja na ishirini
na tano elfu nchini Marekani huweza kufanywa kwa kiasi cha dola elfu 30
tu nchini Mexico.
Sababu nyingine zinazopelekea sekta hii kuimarika
ni kuongezeka umri wa kuishi, na kupewa vibali vya kimataifa kwa
hospitali katika nchi zinazoendelea ambavyo huwa haklikishia wagonjwa
kuwa watakua salama katika hospitali hizo.
Pia bila kusahau maendeleo katika sekta ya teknolojia kwa nchi
zinazoebndelea. Kompyuta huwasaidia wataalam kutambua matatizo ndani ya
muda mfupi.
Lakini pia hatuna budi kuangalia je wagonjwa wanapendezwa
na matokeo katika hospitali fulani, jambo ambalo hupelekea kuongezeka
kwa idadi ya wagonjwa katika nchi fulani.
PUMZIKO 1
Uturuki ni moja ya nchi ambazo imekuwa ikipata idadi
kubwa sana ya wagobnjwa kutoka nje ya nchi na idadi hii imekua
ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Utafiti uliofanywa mwaka 2012 kulingana na rekodi za wagonjwa,
Uturuki inashika nafasi ya 7 kati ya nchi 10 zinazoongoza kwa utalii wa
kiafya duniani. Nchi sita zilizoipita Uturuki ni pamoja na Thailand,
Mexico, Marekani, Singapore,India na Brazil.
Idadi ya wagonjwa wa kigeni ambao walipatiwa matibabu nchini Uturuki
mwaka 2012 ni wagonjwa laki 2 na 70 elfu. Wagonjwa mbalimbali kutoka
nchi 94 tofauti dubniani wamewahi kuja Uturuki na kupatiwa tiba katika
kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Kwa mujibu wa takwimu, idadi kubwa ya wagonjwa wa kimataifa ambayo
Uturuki iliwapata wanatokea katika nchi za Ujerumani, Uholanzi na
Ufaransa.
Wagonjwa waliotembelea Uturuki kwa ajili ya matibabu walitoa sababu
zilizowafanya waje kupata tiba Uturuki kuwa ni pamoja na Ubora wa
matibabu, hali nzuri ya hewa, uwezekano mkubwa wa kula likizo baada ya
tiba, muda mfupi wa kusubiri, na gharama nafuu za matibabu hayo.
Wagonjwa
wengi wamewahi kuitembelea miji ya Istanbul, Ankara na Antalya kwa
ajili ya matibabu. Sekta ambazo zimepokea wagonjwa wengi ni pamoja na
Aesthetiki, Magonjwa ya macho, meno magonjwa ya ndani ya mwili na
magonjwa ya moyo.
PUMZIKO 1
Unaendelea kusikiliza idhaa yako ya kiswahili ya sauti
ya Uturuki na kipindi kilichopo hewani hivi sasa ni Afya, Utalii na
Uturuki. Kama tulivyosema hapo awali kuwa Uturuki ni moja ya nchi ambazo
wagonjwa wengi wa kigeni hupenda kuzitembelea.
Moja ya vivutio
ambavyo wagonjwa huvitembelea ni nishati ya mvuke. Uturuki ni moja ya
nchi saba duniani ambazo zinautajiri mkubwa wa nishati ya mvuke. Kuna
vyanzxo 1500 vya nishati ya mvuke ambavyo joto lake huwa kati ya nyuzi
joto 20 hadi 100.
Utafiti unaonesha kuwa mvuke wa nchini Uturuki una ubora wa hakli ya
juu kutokana na joto lake, na tabia zake za kikemikali na kimaumbile.
Idadi hii kubwa ya vyanzo vya mvuke huwavutia watalii wengi ambao
hutamani kuona. Wengi wa watalii hawa wanatokea barani Ulaya na ni watu
wazee. Katika miaka ya 2000takriban asilimia 17 ya wakazi wa bara la
Ulaya walikua ni wazee wa miaka 65 na kuendelea. Idadi inatarajiwa
kuongezeka na kufikia asilimia 20 ifikapo mwaka 2025.
Watu wengi wa umri huu huhitaji tiba ya kutumia nishati ya mvuke kwa
ajili ya afya zao hivyo hulazimika kwenda nje ya nchi. Mahitaji ya tiba
ya kutumia nishati ya mvuke ni makubwa kwa Ulaya ya Kaskazini na nchi za
Scandinavia ambapo magonjwa ya viungo huwasumbua sana kutokana na
baridi kali.
Kutokana na kuwa na hali ya hewa nzuri, madaktari wenye uzoefu na
waliobobea, Uturuki huwa ndio chaguo la nchi za Ulaya Kaskazini kwa
ajili ya tiba. Jmabon la muhim kabisa ni gharama za matibabu ambazo huwa
juu kwa nchi za Denmark, Ujerumani, Uswidi, na Uholanzi husababisha
idadi ya wagonjwa kuongezeka Uturuki.
Wizara ya Utamaduni na Utalii Uturuki imeweka umuhimu wa kutiosha
katika kuendeleza sekta ya nishati ya mvuke nchini Uturuki. Kuna miradi
mingi ambayo inafanywa ili kuhakikisha kuwa sekta hii inaboreshwa.
Uturuki ina malengo ya kufikisha idadi ya watalii milioni 15 katika
utalii wa sekta ya nishati ya mvuke na kuwa nchio ya kwanza kwa utalii
wa sekta hiyo barani Ulaya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment