Hizo zikiwa ni faida za fenesi hebu sasa tueleze faida za asali,Asali hutengenezwa na nyuki na bila shaka karibu sote tunaelewa kuwa
chakula hicho cha asili ni kina faida nyingi.
Wataalamu wanatuambia kuwa,nyuki ana uwezo wa kutembea maili elfu tatu akikusanya nta za maua ya
aina mbalimbali kutoka katika miti mbalimbali inayoweza kufikia milioni
kumi na tano kwa ajili ya kutengeza asali kilo moja ndani ya miezi
mitatu.
Kutokana na mchanganyiko huu unaotengenezwa na mdudu nyuki,asali ina uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya mia moja.
Kwa sababu hiyo ni bora tukijizoesha kutumia asali badala ya sukari
katika vinjwaji na vyakula mbalimbali hasa kwa kuwa sukari inaweza kuwa
na kemikali zenye madhara kwa miili yetu.
Tunashauriwa kutumia asali
kama kiungo katika chai,uji,maziwa na katika vinywaji mbalimbali
badala ya sukari.
Baadhi pia hutumia asali kama kitoweo kwa kulia ugali
uliopoa.
Si vibaya ukijua kuwa,ukila asali na ugali wa moto unaweza
kupata maumivu ya tumbo.
Tunashauriwa kutumia asali kwa wingi kwani pia
ni 'antibiotics'.Kumbuka kuwa,asali mbichi ambayo haijachemshwa motoni
ndiyo inayofaa.
Sukari iliyoko kwenye asali humeng'enyuka kwa urahisi sana na kugeuka
kuwa glukosi na fruktosi ambayo huingia kwenye damu mwilini haraka sana
ikilinganishwa na vimiminika vingine kama maji ya kawaida.
Asali
husaida pia figo na utumbo kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Asali pia
ina kalori chache sana na ukilinganisha na kiwango cha sukari
ilichonacho,cha ajabu ni kuwa hutoa nishati nyingi katika mwili lakini
haisababishi ongezeko la mwili yaani unene kwa urahisi.
Hata hivyo
tunausiwa kuwa tukitumia asali kiholela na kuila kwa wingi nayo pia
huweza kusababisha unene kama ilivyo sukari.
Faida nyingine za asali ni kusaidia utengenezaji wa damu mwilini,
kusafisha damu na kusaidia mzunguko wa damu kuwa rahisi na mwepesi.
Halikadhalika asali husaidia mishipa ya damu isiathirike na maradhi
yanayoshambulia mishipa hiyo.
Pia husaidia ubongo na kuuweseha kufanya
kazi vizuri na upesi zaidi.
Faida nyingine ya asali ni kusaidia kuua
bakteria wa aina mbalimbali inapotumiwa kwa matibabu na hasa kwenye
vidonda.
Pia asali husaidia kuondoa matatizo ya tishu yaani tissue
difficiency na udhaifu kwenye mwili.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment