Image
Image

Upinzani wambana Dk Migiro,AG bungeni.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha Rose Migiro, jana alibanwa bungeni baada ya wabunge wa upinzani kuhoji juu ya Muswada wa Sheria ya Kulinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi wa mwaka 2015 wakieleza umewahishwa bila sababu yoyote.
Dk Migiro alikutana na kimbuga cha upinzani ikiwa ni siku moja baada ya Bunge la 10 kuigomea Serikali ilipotaka kuingiza bungeni miswada mitatu iliyohusu Wizara ya Nishati na Madini wakisema inahitaji muda mzuri.

Mapema jana, Dk Migiro aliwasilisha ndani ya Bunge muswada huo akilitaka lijadili na kuupitisha ili kutoa nafasi ya kuwalinda watu wa aina hiyo.

Akiwasilisha maoni ya upinzani bungeni, msemaji wa kambi hiyo katika Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu alisema muswada huo hauna tija kwa muda huo kwani unatoa nafasi finyu kwa wabunge kujadili jambo ambalo ni muhimu zaidi kwa wananchi.

Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alisema uharaka wa muswada huo ni kiashiria tosha kwamba Serikali inataka kuminya uhuru wa wabunge kupitia kwa kina sheria hiyo.

“Kanuni zinasema kuwa, sheria inaweza kupitishwa kwa hati ya dharura ikiwa tu kuna mambo ambayo yanataka kutokea ambayo ni pamoja na majanga au vita. Je, kuna uharaka kiasi gani wa kupitisha muswada huu?” alihoji Lissu.

Mbunge huyo mbali na kutoa ufafanuzi katika vifungu vingi katika muswada huo, lakini alisisitiza kuwa ukipitishwa utakuwa umewanyima haki watu wa kada ya chini na kuwapa mwanya viongozi wao.

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alipinga vikali muswada huo pamoja na namna ulivyowasilishwa na akazua mgogoro mkubwa baina yake na Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG), George Masaju.

Malumbano ya wawili hao yalianzia pale Mnyika aliposema kuwa Serikali ni dhaifu katika suala zima la utungaji wa sheria jambo ambalo pia liliamsha hasira za Spika.

Katika hoja zake, Mnyika alipinga jinsi muswada ulivyokuwa ukitoa upenyo kwa watu kutoa taarifa kwa wakubwa wao badala ya kuzipeleka kwa vyombo vingine.

“Mfano, muswada unaelekeza mtu kutoa taarifa kwa kiongozi wake yaani akiwa mfanyakazi wa benki kuu anawezaje kutoa taarifa za ufisadi wa gavana kwa gavana mwenyewe?” alihoji Mnyika.

AG Masaju alipinga kauli za kuwa Serikali inafanya vitu dhaifu akisema siyo nia yao, bali wanafanya kazi ya kupeleka miswada ili wabunge wenyewe ndiyo wafanye uamuzi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment