Wagombea urais kutoka vyama mbalimbali nchini Burkina Faso kusajiliwa Julai 24.
Tume ya uchaguzi ya Burkina Faso CENI, imetangaza kwamba itaanza kupokea stakabadhi za usajili kutoka kwa wagombea urais kuanzia tarehe 24 mwezi Julai.
CENI imetaka vyama vyote vya kisiasa na makundi ya kujitegemea yanayopanga kushiriki kwenye uchaguzi huo utakaofanyika mwezi Oktoba, kuwasilisha stakabadhi zao za usajili ifikapo tarehe 24 mwezi Julai.
Maelezo zaidi yalisisitiza kwamba stakabadhi zote za usajili zinapaswa kuwasilishwa katika afisi ya katibu mkuu wa CENI siku 70 au chache zaidi kabla tarehe ya uchaguzi kufika.
CENI pia imetoa ripoti ya usajili wa wapiga kura uliofanyika kati ya tarehe 3 Machi na tarehe 18 Mei 2015, ambapo watu 892,000 waliweza kusajiliwa kama wapiga kura wapya kote nchini.
Hadi kufikia sasa, watu zaidi ya milioni 5.5 wamesajiliwa kama wapiga kura katika vituo 17,931 vilivyosambazwa kote nchini Burkina Faso.
Uchaguzi wa rais na wabunge utafanyika tarehe 11 mwezi Oktoba 2015, na ule wa manispaa utafanyika tarehe 31 mwezi Januari 2016.
0 comments:
Post a Comment