Image
Image

Wakulima waaswa kuacha kutouza vocha za pembejeo na mbegu zinazotolewa na serkali

Katibu mkuu wizara ya kilimo, chakula na Ushirika SOPHIA KADUMA amewataka wakulima kutouza vocha za pembejeo na mbegu zinazotolewa na serkali kupitia ruzuku ya kilimo kwa wakulima ili wanufaike na ruzuku hiyo kwani kwakufanya hivyo ni kinyume na malengo ya serikali ya kuwawezesha.
Akizungumza katika maonesho ya kilimo na biashara 2015  yanayofanyika katika kituo cha utafiti wa kilimo cha SELIANI, mkoani ARUSHA ,KADUMA amesema ni vema wakulima wakazitumia mbegu zinazotolewa na serikali ambapo pia amewataka wakulima kutumia vizuri elimu wanayoipata kutoka kwa wadau mbalimbali wa kilimo kupitia maonyesho hayo.
Amesema serikali inatoa zuruku kwa wakulima ili waweze kukidhi kilimo cha kisasa na hivyo  ni vema wakazingatia ushauri wa wataalamu hasa katika kutumia mbegu bora na madawa ili kuongeza kipato kwa wakulima.
Mkurugenzi wa utafiti na kilimo kanda ya kaskazini  Dk JANUARY MAFURU, amesema, maonesho hayo  yameshirikisha wadau mbalimbali wa kutoka kanda ya kaskazini na maeneo mengine nchini ili kuwapa fursa wakulima kujifunza zaidi.
Amesema, wameamua kushirikiana na Taasisi za kilimo nchini ili kuwapa wakulima fursa ya kujifunza  kuhusu kilimo bora ikiwa nipamoja na namna yakupata masoko ambapo amesema tayari kuna soko kubwa la mazao jamii ya mikunde.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment