Image
Image

Wanamgambo wa Al-Shabaab waondoka katika mji walioudhibiti kwa miaka mitano nchini Somalia.


Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na vyanzo vya habari, wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab wanaarifiwa kuondoka katika mji wa Bateyri baada ya kikosi cha AMISOM kukaribia eneo hilo.
Wengi wa wanamgambo hao wanasemekana kutorokea katika vijiji jirani na maeneo ya milimani, na kuwaacha wanamgambo wengine wachache mji ni Bateyri.
Kikosi cha AMISOM kinachoshirikiana na jeshi la serikali ya Somalia, kimetangaza kujiandaa kuingia mjini humo ili kuwaondoa wanamgambo wote.
Mji wa Bateyri ulioko katika eneo la Gedo, upande wa kusini magharibi mwa Somalia, ulikuwa ukidhitiwa na kundi la Al-Shabaab kwa kipindi cha miaka mitano.
Kikosi cha AMISOM pamoja na wanajeshi wa Somalia wamekuwa wakitekeleza operesheni na kuikomboa miji kadhaa iliyoko kusini mwa nchi kutoka mikononi mwa Al-Shabaab.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment