Image
Image

Wananchi waaswa kutumia vizuri fedha walizopewa na TASAF kujikwamua kiuchumi.

Waziri wa Nchi ofisi ya rais Mahusiano na Uratibu Dr. MARY NAGU amewataka wananchi mkoani MANYARA kutumia vizuri fedha wanazopewa na  mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF ili ziweze kuwasaidia katika kujikimu na kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza katika uzinduzi wa TASAF awamu ya tatu wilayani HANANG Dr. NAGU amesema wananchi   wanaweza kutumia fedha hizo kuanzisha biashara ndogondogo ambazo zitapelekea kuongezeka kwa pato lao.
Watu ELFU TANO katika wilaya wa HANANG  wanatarajia kunufaika  na fedha hizo.
Hivi karibuni mkurugenzi mtendaji waTASAF LADISLAUS MWAMANGA alitangaza kuanza kutoa fedha za uhawilishaji kwa wananchi wa mikoa 4 ambayo ni MANYARA, ARUSHA, MARA na KILIMANJARO.
TASAF inatoa fedha kwenye halmashauri 27 za mikoa hiyo ambapo inakadiriwa jumla ya zaidi ya Bilioni 6 zinatolewa kwa wananchi na mfuko wa TASAF katika kusaidia wananchi kupambana na umasikini
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment