Mamia ya watu pia walilazimika
kuondolewa karibu na eneo hilo ili kuepuka athari ya kemikali hiyo
iliyovuja.
Kemikali hiyo aina ya ‘Sulfur Dioxide’ ilivuja katika kiwanda
cha Hydrite Chemical Company usiku wa jumamosi , na kutapakaa katika
eneo lililokuwa na umati wa watu uliokuwa ukitazama mashindano ya magari.
Watu takriban 300 waliondolewa
kwenye eno hilo huku wengi wao wakilalamika kuwa na matatizo ya kupumua.
Watu 15 walioathirika vibaya
walipachikwa vipumulio vya hewa ya oksijeni na kufikishwa katika hospitali ya Terre
Haute.
0 comments:
Post a Comment